Monday, October 29, 2012

TAMASHA LA PENUEL TAG KIGOGO MBUYUNI LAFANA

linaloongozwa na Mch Linde lilijaa watu hata kukawa hakuna sehemu ya kukaa. kwaya mbalimbali ziliimba katika tamasha hilo. kwaya hizo ni kama Revival Magomeni, Kwaya ya watoto Magomeni, Kwaya ya diodoxer ya Magomeni Christ Boyz band ya Magomeni TAG na kulikuwepo na kwaya ya wenyeji  kwaya kutoka Msasani TAG, kwaya ya EAGT Kigogo kwaya ya TAG Tandale kwa Mch Mshama, na waimbaji binafsi kadha wa kadha.



Mgeni rasmi akiingia kanisani


Mc wa Tamasha hilo ndugu Tony akicheza



Mr& Mrs Mwakibuti ambaye alikuwa mgeni rasmi mchungaji Linde 


watu wakiwa wamejaa mpaka nje ya kanisa

katika Tamasha hilo mgeni lasmi alikuwa ni Makamu mkurugezi CA's jimbo la mashariki Ndugu Joseph Mwakibuti. ambapo lengokubwa ilikuwa ni kuchangia ununuzi wa viti vya kanisa hilo

ZAKAYO MAGULU CAMERA MAN NO 1 TANZANIA KUANDAA TAMASHA LA KUREKODI DVD LIVE DEC 23 MWISHO WA MWAKA HUU

     
Jina la zakayo Magulu si geni hasa wale waangaliaji wa kwaya na movie za Marehemu kanumba. mimi nilimfahamu alipoturekodi mkanda wa kwaya yetu ya Revival Magomeni kipindi hicho akiwa na Mtitu Game na akawa ana record movie na baadae akawa anafaya kazi ya kurekodi filamu za marehemu Kanumba. na katika blog ya kanumba the great aliwahi kusema kuwa Zakayo he the best camera man in Tanzania. nami naamini kutokana na kazi nyingi ambazo amezifanya na anaendelea kuzifanya. na hata DVD ya sifa zivume ya John Lisu ni moja ya camera man waliorekodi. sasa mwaka huu anakuja kivingine kabisa kwani yeye mwenyewe sasa ana andaa tamasha kubwa la kisasa kwani vitatumika technolojia mpya katika kuboresha DVD hiyo iwe kwenye viwango vya kimataifa. katika ukurasa wake wa fb ameandika hivi
MY BROTHERS $ SISTERS NINAPENDA KUWAJULISHA KUWA TAREHE 23 DEC 2012 NATEGEMEA KUFANYA LIVE CONSERT RECORDING...UKUMBI NI MAKUMBUSHO YA TAIFA POSTA MKABALA NA IFM.CONSERT ITAANZA SAA 9 ALASILI MPAKA SAA 1 JIONI, TEGEMEA KUKUTANA NA BWANA....LAKINI PIA KUWAONA NA KUSALIMIANA NA WATU AMBAO SI RAHISI KWA MBANANO WA MAJUKUMU KUKUTANA NAO